Search This Blog

Wednesday, October 13, 2010

http://news.yahoo.com/video/abcplus-22309221/abc-news-plus-22309266

Monday, October 4, 2010

''TUTAISHI KWA MATUMAINI HADI LINI?''......Sauti ya Mtanzania aliyezongwa na ahadi kemkem ambazo mwisho wa siku huwa kama ndoto za Alinacha


Wakati nchi yetu ikiwa katika mchakato wa kujiandaa na kuwapigia kura Madiwani, Wabunge na nafasi ya Urais, kuna mambo mengi yamekuwa yakitokea mojawapo ni utitiri wa ahadi kutoka kwa wagombea.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa viongozi kutoa ahadi nyingi wakati wa kuomba kura kutoka kwa wananchi kitu ambacho kimedhihirika kwamba asilimia kubwa ya mambo yaliyoahidiwa yangetekelezwa, mara nyingi huishia kuwa  hadithi za sungura na fisi..

Ni dhahiri suala la kutoa ahadi hewa kwa wananchi ni jambo lisilo lakiungwana na pia kimaadili kutokana na ukweli kwamba kiongozi anakuwa amepewa dhamana ya kuwaongoza wananchi na kuaminiwa kusimamia rasilimali zao dhidi ya wabadhirifu wa ndani na pia nje. Hivyo basi jamii inatarajia kwamba kiongozi atakuwa ni mtu mwema na pia atakuwa ndiye kichocheo cha maendeleo katika nyanja mbalimbali.


Hii ni changamoto kwa Tume ya Uchaguzi kutafuta njia ambayo kwayo itakuwa muafaka kuweza kusimamia yale yaloahidiwa majukwaani, ili yatekelezwe kama yalivyotamkwa na wagombea. Pia kwa utaratibu huo huo itasaidia kuwapa wananchi nafasi ya kuwahoji viongozi mara tu kipindi chao cha miaka mitano kinapokuwa kimefikia ukingoni wakiwa katika harakati za kuomba kupewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kingine. Kwa kufanya hivyo litakuwa jambo la maana si  tu kwa maendeleo ya nchi bali hata heshima ya kiongozi husika na chama anchokiwakilisha.

Kutokana na hali hiyo nivyema ingeundwa Tume itakayofatilia na kuhakikisha ahadi zote zinazotolewa na wagombea katika majukwaa ya siasa zinatekelezwa kwa ukamilifuili isije ikawa danganya toto. Tanzania yenye neema inawezekana na inaanza na Kiongozi anayemaanisha kile asemacho.

Saturday, October 2, 2010

NANI TUMTALAJIE KUWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUPIGA KURA ZETU ZA NDIYO KWA HAWA WAGOMBEA WATATU.....!!!!?? Mwananchi hakikisha siku ya tarehe 31/10/2010 unaenda kupiga kura katika kituo ulichojiandikisha. Tanzania yenye neema na matumaini inawezekana na inaanza na wewe kwa kutumia vyema haki yako ya kikatiba kumchagua kiongozi bora na si bora kiongozi....UKIFANYA KOSA KATIKA KUCHAGUA MGOMBEA, KULISAHIHISHA NI MPAKA MIAKA MITANO IJAYO HIVYO NI JUU YAKO KUAMUA!!!!!

Dk. Slaa ni nani hasa? Jinale kamili ni Wilbrod Peter Slaa, aliyezaliwa siku ya Ijumaa, Oktoba 29, 1948. Alisoma Shule ya Msingi Kwermusl iliyopo Mbulu kati ya 1958 na 1960 kabla ya kuhamia Shule ya Msingi Daudi mwaka 1961 na baadaye Shule ya Msingi Karatu kuanzia 1962 hadi 1965.

Baada ya hapo alijiunga Seminari ya Dung'unyi kuanzia 1966 hadi 1969 kwa elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne, kabla ya kwenda Seminari ya Itaga mkoani Tabora kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita 1970.

Baada ya hapo alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho, Moshi, alikosomea Falsafa kati ya mwaka 1972 na 1973 na kupata cheti. Alijiunga Seminari ya Kipalapala mwaka 1974 na kupata cheti katika Theolojia mwaka 1977.

Slaa alikwenda Chuo Kikuu cha Mtakarifu Urban kilichopo Roma, Italia, alikosoma hadi mwaka 1981 na kupata Phd. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas Aquinas na kujipatia Stashahada ya Uzamili katika Maendeleo Vijijini.

Mwaka 1985 alitunukiwa Cheti katika Menejimenti kutoka TransWorld Tutorial College, London, Uingereza wakati mwaka 1993 alijipatia cheti baada ya kuhudhuria kozi ya Afya ya Macho.

Amefanya kazi wapi? Alikuwa Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadi 1991; Mkurugenzi wa Maendeleo wa Jimbo la (Kanisa) Mbulu 1977 hadi 1991; Msaidizi wa Askofu (1982 – 1991); Mkurugenzi wa Maendeleo Jimbo la Mbulu (1982 – 1985); Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (1985 – 1991); Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wasioona Tanzania, nafasi aliyokuwa nayo kuanzia 1992 hadi 1998.

Uzoefu wake katika siasa unaanzia katika chama cha Tanganyika African National Union (Tanu), akiwa Mwenyekiti wa Tawi la Tanu Kipalapala 1974; Katibu wa Umoja wa Vijana wa Tanu 1974 na baadaye Katibu wa CCM (Tawi la Nje – Roma, Italia) 1980 – 1982.

Baada ya hapo alijiunga na Chadema, ambapo mwaka 1995 alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chadema na baadaye mwaka huo huo akawa Mbunge wa Karatu, nafasi anayoshikilia hadi sasa.

Mwaka 1998 alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema na mwaka 2002 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, nafasi anayoshikilia hadi sasa, anapojitosa kuwania urais wa Tanzania.
HISTORIA YA PROFESA LIPUMBA
Ukiongelea wanasiasa wenye taaluma zinazoeleweka nchini Tanzania,sio ajabu mojawapo ya majina yako ya mwanzo mwanzo litakuwepo la Profesa Ibrahim H.Lipumba.(pichani). Lipumba ni Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama Cha Wananchi,CUF.

Alizaliwa tarehe 6 Juni mwaka 1952 katika kijiji cha Ilolangulu,wilaya ya Tabora Vijijini mkoani Tabora,Tanzania. Alianza elimu yake ya msingi (1959-1962) katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School huko Sikonge Tabora. Kuanzia mwaka 1962 mpaka 1966 alikuwa L.A Upper Primary School huko huko Sikonge,Tabora.

Baadaye aliendelea na masomo ya sekondari (1967-1970)-Tabora Boys Secondary School na baadaye (1971-1972) Pugu Secondary School. Mwaka 1973-1976 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam ambapo alipata Shahada ya kwanza (BA Economics). Mwaka 1976-1978 alikuwa tena Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya Shahada ya pili (MA Economics).Baadaye alielekea Stanford University nchini Marekani (1978-1983) alikosomea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kwenye masuala hay ohayo ya Uchumi.

Hii ndio inayomfanya Lipumba kuwa mmojawapo wa wachumi wanaoheshimika barani Afrika kama sio ulimwenguni. Kwa habari zaidi juu Profesa Ibrahim Lipumba na habari za uzoefu wake katika uongozi,nafasi za kazi alizowahi kushikilia,heshima za kitaaluma alizonazo, shughuli za kimataifa alizowahi kufanya nk bonyenza hapa. CV yake unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa.
HISTORIA YA KIKWETE
Jakaya Mrisho Kikwete tangu tarehe 21 Desemba 2005 ni rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amezaliwa 7 Oktoba, 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
MASOMO
1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza digrii yake mwaka 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
KUPANDA NGAZI KATIKA SIASA
1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka. 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwl. Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia Benjamin Mkapa nafasi aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri ya Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.

FANUEL SEDEKIA - Niwewe bwana!!!!!